NAFASI ZA KUJITOLEA MASHINDANO YA CHAN

Posted 2 days ago

Mashindano ya CHAN 2024 yanatarajiwa kufanyika hapa Tanzania kuanzia tarehe 1– 28 Februari 2025.

  • Wanahitajika watu wenye ari na uzalendo wa kujitolea ili kufanikisha tukio hili kubwa na la kimataifa.
  • Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi mwenyeji wa mashindano haya, tunatoa nafasi za kujitolea kwa vijana  wenye utayari wa kutoa muda na nguvu zao kusaidia maandalizi na utekelezaji wa mashindano haya.

SIFA ZA MWOMBAJI

  • Awe raia wa Tanzania
  • Umri wa miaka 18 hadi 40
  • Awe na utayari wa kujitolea muda wake na kufanikisha mashindano.
  • Mwenye kiwango cha elimu ya kidato cha IV na kuendelea.
  • Mwenye ufasaha wa kuzungumza lugha ya Kiswahili na Kingereza
  • Mwenye uwezo wa kupatikana muda wote
  • Awe na mawasiliano mazuri na uwezo wa kufanya kazi katika mazingira ya timu.
  • Ujuzi wa ziada kama lugha za kigeni, teknolojia, au uzoefu katika mashindano ya michezo utazingatiwa kama nyongeza za sifa.
  • Barua kutoka ofisi za Serikali ya Mtaa unayoishi kwa sasa.

Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi haya ni tarehe 13 Januari 2025. Asante kwa nia na ushirikiano wako. Tunatazamia kukukaribisha kwa timu yetu ya kujitolea!

Nafasi za kazi

Mwisho Kupokea Maombi

13, Januari 2025

Jaza hapa chini kuomba nafasi

A valid phone number is required.
A valid email address is required.